.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 7 Agosti 2014

KESI YA PISTORIUS PANDE ZINAZOHUSIKA KUKAMILISHA MALUMBANO

Kesi ya mauaji inayomkabili mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius inatarajiwa kukamilisha malumbano ya kisheria baada ya kumalizika kwa utoaji wa ushahidi katika kesi hiyo inayofuatiliwa mno na vyombo vya habari vya ndani na nje.

Mwendesha mashtaka Gerrie Nel atakuwa wa kwanza kumalizia kutoa maelezo yake, ambapo upande wa utetezi nao utafuatia kufanya hivyo hapo kesho.

Mwanariadha huyo mlemavu amekanusha kumuua kwa makusudi rafiki yake wa kike mwanamitindo Reeva Steenkamp Februari 14 mwaka jana na kudai kuwa alidhani kuwa ni mtu aliyevamia nyumbani kwake.
                           Reeva akiwa na mpenzi wake Pistorius wakati wa uhai wake

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni