.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 21 Agosti 2014

MANCHESTER UNITED YAFANIKIWA KUMNASA BEKI WA SPORTING LISBON

Timu ya Manchester United imethibitisha kunasa saini ya mchezaji wa Sporting Lisbon beki Marcos Rojo kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 16.

Rojo, ambaye alitua jumanne jioni Jijini Manchester na kusema kujiunga na Manchester United kwake ni sawa na kukamilisha ndoto yake ametia saini jana mkataba wa miaka mitano baada ya kufaulu vipimo na kukubaliana na maslahi yake.

Kocha Louis van Gaal amehakikisha kuwa anamnasa beki huyo anayetumia mguu wa kushoto, kufuatia kupata kipigo jumamosi kutoka kwa Swansea, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni