.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 21 Agosti 2014

WALIOPOTEZA MAISHA KUTOKA NA MAPOROMOKO YA ARDHI NCHINI JAPAN WAFIKIA 39

 Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Japan imefikia 39 huku msako wa kuwatafuta watu wengine waliopoteza maisha ukiendelea kwa kasi. 

Idadi hiyo ya waliopoteza maisha imeongezeka kufuatia msako wa kuondoa vifusi katika maeneo hayo yaliyokumbwa na maporomoko katika safu za milima ya Hiroshima.
 Shirika la utabiri wa hali ya hewa la Japan limesema maporomoko hayo kwenye milima ya Hiroshima yalisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa saa 24 na ambayo ilikuwa ni sawa na mvua iliyonyesha kwa muda wa mwezi mmoja mfululizo.
 Picha toka eneo la tukio zinaonyesha nyumba zikiwa zimefukiwa na matope pamoja na mawe yaliyotokana na maporomoko hayo, wakati vikosi vya uokoaji vikiwa vinaelekea katika nyumba zilizobomolewa na kufunikwa na matope.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni