Marekani imefanya mashambulizi katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi wa kundi la ISIS nchini Iraq ikiwa ni hatua yake ya kuwalinda raia wa Marekani waliopo katika maeneo hayo.
Mashambulizi hayo yamefanywa jana na ndege za kivita za Marekani ambapo zilishambulia vifaru vya wanamgambo hao wa Kiislam ambao hivi sasa wanashikilia eneo kubwa nchini Iraq.
Wanamgambo hao wamekuwa wakifanya mauaji ya mara kwa mara kwa raia, na hivi sasa wamewafanya raia ambao ni wakristo kukimbia makazi yao kufuatia hatua yao ya kutaka kuwashambulia.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni