.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 6 Agosti 2014

MAREKANI YATEKELEZA ADHABU YA KIFO KWA MWANAUME MMOJA HUKO MISSOURI

Mwanaume mmoja nchini Marekani ametekelezewa adhabu yake ya kifo katika jimbo la Missouri baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka na kumuua mwanafunzi wa chuo mnamo mwaka 1995.

Adhabu hiyo imetekelezwa kwa Michael Worthington, 43, ni ya kwanza kutekelezwa Marekani tangu mwezi uliopita, ambapo dawa ya sindano ya kifo kwa mfungwa huko Arizona ilipochukua muda wa saa mbili kabla ya kufa.

Worthington alikiri kumshambulia, kumbaka na kumuua mwanafunzi Melinda Griffin, 24, akiwa nyumbani kwao. Ilimchukua muda wa dakika 10 kabla ya Worthington kufa baada ya kuchomwa sindano hiyo ya kifo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni