.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 1 Agosti 2014

MERIAM NA MUMEWE HATIMAYE WAWASILI NCHINI MAREKANI

 Mwanamke aliyekuwa amefungwa gerezani nchini Sudan kwa kubadili dini kutoka Uislamu hadi Ukristo, Meriam Ibarhim hatimaye amewasili jana nchini Marekani na kupokelewa kwa furaha na ndugu, jamaa na marafiki waliofika kuwapokea yeye na mumewe Daniel Wani aliyekuwa katika kiti cha magurudumu pamoja na watoto wao wawili. 

Meriam alihukumiwa kunyongwa mapema mwaka huu na mahakama nchini Sudan baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kubadili dini, alisalimika baada ya mataifa mbalimbali ulimwenguni ikiwemo Marekani kupinga hukumu hiyo. 

Meriam na mumewe ni wazaliwa wa Sudan lakini wenye uraia wa Marekani.
 Akiwa gerezani alijifungua mtoto wake mdogo, na hata alipotoka gerezani bado alikumbana na vikwazo mbalimbali kabla ya kupata hifadhi katika ubalozi wa Marekani nchini Sudan. 

Baadaye alifanikiwa kuondoka nchini humo na kuelekea Rome, Italia ambako huko alikutana na kiongozi wa Kanisa Katoliki Dunia, Papa Francis, na hadi kuwasili Marekani jana alhamisi alikuwa akitokea Italia yeye na familia yake.
 Walipowasili nchini Marekani, walipokelewa kwa furaha na ndugu na jamaa zao, hali iliyomfanya mumewe Meriam, Daniel Wani atokwe na machozi mfululizo.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni