.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 11 Agosti 2014

MKE WA WAZIRI MKUU MAMA TUNU PINDA AKIWA KATIKA MKUTANO WA DUNIA KUHUSU AMANI NA USALAMA, JIJINI SEOUL


Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akifuatilia mada iliyowasilishwa leo asubuhi (Agosti 11, 2014) kuhusu amani na usalama barani Afrika katika Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaendelea jijini Seoul, Korea Kusini (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).


Balozi wa Kudumu wa AU kwenye Umoja wa Mataifa, Bw. Antonio Tete akitoa mada kuhusu amani na usalama barani Afrika leo asubuhi (Agosti 11, 2014) katika Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaendelea jijini Seoul, Korea Kusini. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM)


Mjumbe wa Baraza la Uendeshaji la UNESCO, Dk. Mary Mbiro Khimulu akitoa mada kuhusu amani na usalama barani Afrika leo asubuhi (Agosti 11, 2014) katika Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaendelea jijini Seoul, Korea Kusini. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).


Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (kulia) akisalimiana na Rais wa Shirikisho la Wanawake na Amani Duniani (WFWP), Prof. Yeon Ah Moon, wakati akisubiri kushiriki mkutano wa shirikisho hilo kwenye ukumbi wa Jumba la Makumbusho la Kimkoo, jijini Seoul, Korea Kusini leo mchana (Agosti 11, 2014). Katikati ni mke wa Rais wa zamani wa Uruguay, Bibi Mercedes Menafra de Batlle. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM)


Baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku moja ulioandaliwa na Shirikisho la Wanawake na Amani Duniani (WFWP), wa kwanza mstari wa mbele ni Rais wa WFWP, Prof. Yeon Ah Moon akifuatiwa na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Dk. Lan Young Moon kwenye ukumbi wa Jumba la Makumbusho la Kimkoo, jijini Seoul, Korea Kusini leo mchana (Agosti 11, 2014). (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM)


Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa tatu kushoto) akiwa na viongozi wakuu wakifuatilia mada kwenye mkutano wa siku moja ulioandaliwa na Shirikisho la Wanawake na Amani Duniani (WFWP) kwenye ukumbi wa Jumba la Makumbusho la Kimkoo, jijini Seoul, Korea Kusini leo mchana (Agosti 11, 2014). Kutoka kushoto ni Balozi wa Uruguay nchini Korea, Alba Rosa Legnani, Mke wa Rais wa visiwa vya Marshall, Bibi Lieom Anono Loeak na wa kwanza kulia ni mke wa Rais wa zamani wa Uruguay, Bibi Mercedes Menafra de Batlle. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM)


Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (wa pili kulia) akiwa na viongozi wa Shirikisho la Wanawake na Amani Duniani (WFWP) pamoja na wake wa Marais mara baada kumaliza mkutano wa siku moja ulioandaliwa na Shirikisho hilo kwenye ukumbi wa Jumba la Makumbusho la Kimkoo, jijini Seoul, Korea Kusini leo mchana (Agosti 11, 2014). (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni