.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 7 Agosti 2014

NDEGE YATUA KWA DHARURA KWENYE UWANJA WA JESHI BAADA YA INJINI KUZIMWA

Ndege iliyokuwa imejaa abiria wakielekea Manchester imelazimika kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa jeshi unaolindwa kwa silaha huko Azores baada ya injini yake moja kuzimwa.

Wakati hitilafu hiyo ikitokea ndege hiyo ya Thomson Airways Boeing 787 Dreamliner
ilikuwa na abiria 288 wanaotokea Jamhuri ya Dominica ambapo waliambiwa na rubani injini moja itazimwa kutokana na hitilafu.

Baada ya kutolewa taarifa hiyo abiria waliambiwa ndege itatua kwa dharua katika uwanja ulipo karibu na baada ya kusafiri ikiwa kima cha chini kwa saa nne, walielezwa wajiandae kutua katika mazingira magumu kwenye uwanja huo wa jeshi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni