.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 7 Agosti 2014

MWENDESHA MASHTAKA ASEMA OSCAR PISTORIUS AMEIELEZA MAHAKAMA RUNDO LA UONGO

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ameshutumiwa kwa kuwa shahidi muongo ambaye ameiambia mahakama rundo la maelezo ya uongo, kauli ambayo imetolewa wakati wa kukamilisha malumbano ya kisheria ya kesi ya mauaji inayomkabili.

Wakati Pistorius akikanusha kumua kwa makusudi mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa madai ya kufikiri kuwa ni mtu aliyevamia nyumbani kwake, hata hivyo mwendesha mashtaka amesema alimuua kwa makusudi baada ya kugombana.

Mwendesha mashtaka huyo Gerrie Nel, ametoa maelezo hayo wakati akikamilisha kutoa maelezo yake katika kesi hiyo hii leo, kabla nao upande wa utetezi kutoa maelezo yake hapo kesho.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni