Padri raia wa Hispania amekuwa ni
mtu wa kwanza aliyeugua Ebola kurejeshwa nyumbani barani Ulaya kwa
ajili ya matibabu hii leo.
Padri Miguel Pajares, amekimbizwa
hospitali Jijini Madrid, baada ya kubebwa kwa ndege ya jeshi akitokea
nchini Liberia leo asubuhi.
Mmishenari huyo alibidi atengwe na
watu tangu jumamosi, baada ya kubainika anavirusi vya ugonjwa hatari
wa Ebola.
Padri Pajares, ambaye alikuwa
akitibu wagonjwa wa Ebola katika hospitali inayo milikiwa na Kanisa
Katoliki, amerejeshwa na sista aliyeambatana nae ambae naye yupo
chini ya uangalizi wa madaktari ingawa hajaambukizwa virusi vya
ugonjwa huo.
Picha ya ndani ya ndege ya jeshi iliyombeba Padri Pajares
Vilio vikiwa vimetawala kwa ndugu na jamaa wenye wagonjwa wa Ebola

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni