Jasusi wa Marekani aliyeomba hifadhi
baada ya kuvujisha siri za taifa lake amepewa ruhusa ya kuendelea
kuishi Urusi kwa miaka mitatu zaidi.
Jasusi huyo Edward Snowden muda wake
wa kuishi nchini Urusi ulikuwa umeisha tangu Julai 31, mwaka huu.
Snowden alikimbia Marekani tangu
mwaka 2013 baada ya kuvujisha siri za Usalama wa Taifa wa Marekani
zinazohusu udukuzi wa maongezi ya simu ya viongozi wa mataifa
mengine.
Marekani imemfungulia Snowden
mashtaka ya kuiba mali za serikali pamoja na kutoa siri nyeti za
taifa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni