.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 6 Agosti 2014

NJAA YAUWA WATU WANNE HUKO BARAGOI NCHINI KENYA

Watu wanne wamekufa kwa njaa huko Baragoi, kaunti ya Samburu kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Chama cha Msalaba Mwekundu nchini Kenya.

Mratibu wa chama hicho Gitonga Mugambi katika ukanda huo ameviambia vyombo vya habari mzee mmoja amekufa wiki iliyopita.

Hata hivyo wakazi wa eneo hilo wamedai watu saba wamekufa kwa njaa, miongoni mwao wapo wanawake wanne, mtoto mmoja na wanaume wawili katika eneo la Logetei huko Baragoi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni