Rais wa Liberia Ellen Johnson
Sirleaf ametangaza hali ya dharura wakati taifa hilo likikabiliwa na
mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Akiongea kwenye televisheni ya taifa
amesema baadhi ya uhuru wa raia kujifanyia mambo watakavyo
utasitishwa.
Ugonjwa wa Ebola umezikumba nchi za
Guinea, Sierra Leone na Nigeria, huku ukiuwa watu zaidi ya 930.
Wataalam wa Shirika la Afya Duniani
(WHO) wanakutana Jijini Geneva nchini Switzerland, kujadili namna ya
kukabiliana na mlipuko huo mkubwa kuwahi kutokea.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni