.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 27 Agosti 2014

URASIMU KUSABABISHA MAKALI YA KUKOSA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA NCHINI KENYA


    Mgonjwa akichungulia nje kuangalia madaktari waliogoma na kuwatelekeza 

Makali ya kuchelewa kwa Baraza la Seneti na Bunge la Taifa katika kupitisha muswada muhimu kwa kaunti yataendelea kuwapata watumishi wa umma kwa kukosa mshahara wao wa mwezi huu.

Huu utakuwa ni mwezi wa pili kwa watumishi wa umma kubeba mzigo wa urasimu wa kutengwa fungu la fedha kwa ajili ya kuendesha serikali za kaunti.

Hali hiyo ya kuchelewesha mishahara imepelekea kuibuka mgomo wa madaktari Mombasa ambao umepelekea kusababisha vifo vya wagonjwa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni