.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 22 Agosti 2014

WANACHAMA COASTAL UNION WATAKA UCHAGUZI MKUU

WANACHAMA wa Klabu ya Coastal Union bado wameonyesha nia ya kutokumkubali Makamu Mwenyekiti wa klabu,Steven Mguto hiyo na kuomba uitishwe mkutano mkuu wa uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi mitatu ili kuweza kuzipa mapengo ya nafasi zilizopo wazi.


Nafasi hizo ni Mwenyekiti na Wajumbe wawili ili kuweza kuongeza nguvu katika utendaji wa klabu hiyo lengo likiwa kuharakisha kasi ya maendeleo na ufanisi hasa kwa viongozi wa ngazi za juu.

Hayo yalielezwa jana na Wanachama hao wakati wa kikao cha pamoja mbele ya Mwanasheria kutoka ndani ya shirikisho la soka nchini (TFF) anayeshughulikia masuala ya Uanachama, Eliud Msovela wakati alipokuwa akipokea maoni ya wanachama wa timu hiyo.

Mmoja kati ya wanachama hao Salim Perembo amesema kimsingi baada ya kufanyika uchaguzi huo na kupatikana Mwenyekiti wa wajumbe hao itamuongezea nguvu kwenye safu ya uongozi kufanya kazi zake ipasavyo na kwa ufanisi mkubwa kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya timu hiyo.

Perembo amesema uchaguzi huo kufanyika utatoa mwelekeo mzuri wa kuendelea kupata viongozi ambao watakuwa na madaraka kamili hali itakayoongeza umakini na uwajibikaji kwenye utendaji wa shughuli za siku kwenye klabu hiyo.

Naye mwanachama mwengine Yunusu Makata ambaye mwenye kadi nambari 245 alisema kujazwa kwa nafasi za uongozi zilizowazi utaiwezesha klabu hiyo kuimarika hasa kwenye eneo hilo na hatimaye kuiwezesha kupata maendeleo kwa kuweka mipango imara itakayoleta mafanikio siku za usoni.

Kwa upande wake mwanachama Salimu Mazrui mwenye kadi namba 0201, alisema suala la uchaguzi huo ni la muhimu sana kwa ajili ya kuimarisha safu za juu za uongozi ngazi ya klabu hiyo baada ya kuonekana kushindwa kusimamia ipasavyo majukumu yao .

Alisema wanachama hao ndio waliamua kukubaliana na kauli moja ya kusema kuwa Makamu Mwenyekiti huyo hafai kuongoza kwenye klabu hiyo kutokana na kuvunja katiba kitendo ambacho kimepeleka wanachama kukosa imani naye.

Hata hiyo mwanachama mwengine,Hemed Mbaraka ,Coastal Union inaendeshwa na katibu yake lakini Steven Mguto hafuati katia ua Coastal Union na sio muadilifu kwenye uongozi wake hivyo yeye binafsi hana imani naye na kutaka endele kuwepo kwenye nafasi hiyo hiyo ya kudumazwa mpaka atakapojirekebisha.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Msovela alisema kuwa klabu hiyo inatakiwa kuhakikisha inafanya marekebisho ya katiba kwa sababu hilo ndio jambo ambalo linaokena halijakaa sawa sawa .

Alisema kama katiba hiyo ingekuwa imerekebishwa inawezekana kumuwajibisha kiongozi wa ngazi za juu kwenye kamati ya maadili kipindi anapofanya mambo yasiyokuwa mazuri ndani ya klabu badala ya kutumia neno la kumdumaza.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni