Vikosi vya Ulinzi vya nchini Liberia
vimesambazwa katika Jiji la Monrovia kusimamia marufuku ya kutotoka
mtu kwenye kitongoji kikubwa cha makazi duni katika jitihada za
kudhibiti ugonjwa hatari wa Ebola.
Hatua hiyo imechochea maandamano ya
kupinga marufuku hiyi kutoka kwa wakazi wa kitongoji hicho cha West
Point ambapo watu wamekusanyika katika vizuizi vya barabarani
kulalamikia agizo hilo.
Rais Ellen Johnson Sirleaf pia
ameagiza kutotoka nje watu usiku ikiwa miongoni ya mikakati ya
kukabiliana na Ebola, ambayo imeua watu 1,350 tangu kutokea mlipuko
wake kwenye nchi nne za Afrika ya Magharibi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni