Kumeza kidonge cha aspirin kila siku
kunapunguza nafasi ya kufa kutokana na saratani ya utumbo mdogo ama
utumbo mkubwa.
Wanasayansi wamebashiri kuwa iwapo
kila mtu mwenye umri wa miaka 50 na kuendelea huko Uingereza angemeza
dawa ya aspirin kwa miaka 10, vifo 122,000 vingeweza kuzuilika katika
miongo miwili.
Hata hivyo wanasayansi hao wameonya
kuwa umezaji wa aspirin, unaweza sababisha utumbo kutoka damu, hivyo
ushauri wa madaktari unahitajika kabla ya kuanza kuitumia dawa hiyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni