.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 2 Agosti 2014

WATU WAWILI WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA BASI LA HOOD KUGONGANA NA BASI DOGO JIJINI ARUSHA

Watu wawili wamefariki dunia na wengine 14 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Hood kugongana uso kwa uso na basi dogo katika eneo la Makumira wilayani Arumeru mkoani Arusha .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amewataja waliopoteza maisha kuwa ni pamoja na dereva wa basi dogo aliyejulikana kwa jina la  Jumanne Mohamed na abiria aliyejulikana kwa jina la Anaret Sabas.

Mganga mkuu wa wilaya ya Arumeru walikolazwa majeruhi Dr, Azizi Msuya amesema majeruhi wanaendelea na matibabu na kwamba baadhi yao wamepelekwa katika hosipitali ya mkoa ya Mount Meru .

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema imetokea baada ya basi la Hood kutaka kulipita gari lingine .
Basi la Hood lilikuwa linatoka Arusha kwenda Mbeya na basi dogo aina ya Hiace lilikuwa linatoka Usa river kwenda jijini Arusha

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni