.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 27 Agosti 2014

WAZIRI CHIKAWE AKUTANA NA MWANAHARAKATI WA KIMATAIFA WA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO, GRACA MACHEL JIJINI DSM LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (Kushoto) akizungumza na Mwanaharakati wa Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe alimueleza Mama Machel, juhudi zake za kuingiza katika Katiba Mpya kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya miaka 18 asioe wala asiolewe.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe amekutana na Mwanaharakati wa Kimataifa wa haki za wanawake na watoto, Graca Machel na kujadili masuala mbalimbali ya haki za wanawake na watoto katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.

Katika mazungumzo yao, Waziri Chikawe alimwambia mke huyo wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, juhudi zake za kuingiza katika Katiba Mpya kifungu cha kuzuia mtoto wa chini ya miaka 18 asioe wala asiolewe.

Hata hivyo, Mama Machel kwa upande wake alimshukuru Waziri Chikawe kwa maoni yake na kusema kuwa ni muhimu kwa wadau wote wa haki za watoto wakashinikiza wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na watunga sheria wote wahakikishe kipengele hicho kinaingia ndani ya Katiba. Mama Machel yupo nchini kuhudhuria mkutano wa ufunguzi wa Kampeni ya Kitaifa
ya kutokomeza ndoa za utotoni.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni