.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 30 Agosti 2014

WAZIRI MKUU ASISITIZA UMOJA KWA MAJESHI YA EAC

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hayana budi kuendeleza umoja na mshikamano ili kukuza udugu uliopo.

Ametoa kauli hiyo jana usiku (Ijumaa, Agosti 29, 2014) wakati akifunga mashindano ya Michezo ya Majeshi ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye Uwanja wa Amaan, mjini Zanzibar.

Waziri Mkuu ambaye kabla ya kuhutubia umati ulioshiriki hafla hiyo, alikabidhi kombe kwa washindi wa soka, ambao ni timu ya Jeshi la Ulinzi la Kenya, alisema amefarijika kwa jinsi alivyoshuhudia mechi kati ya Tanzania na Uganda ikichezwa kwa staha bila vurugu zozote. Katika mechi hiyo, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 na kuifanya Tanzania iibuke mshindi wa pili kwenye mchezo wa soka na Uganda kushika nafasi ya tatu.

“Michezo siyo chuki bali hujenga uelewano na mshikamano. Ni fursa ya kujenga mahusiano ya baadaye kwani hakuna ajuaye, huenda tukawa na jeshi moja la Jumuiya huko mbele,” alisema.

Alisema kutokana na ustadi ulioonyeshwa na wachezaji, wakuu wa majeshi waangalie uwezekano wa kutafuta mechi na jumuiya nyingine za Afrika Magharibi ama Afrika Kaskazini ili kujipima kwa kiwango kikubwa zaidi badala ya wao kwa wao. “Tujaribu kwenda nje ya Jumuiya yetu tukashindane nao kwa sababu nimeona uwezo mnao,” alisema.

Katika mashindano hayo yaliyoanza Agosti 19, 2014, Kenya iliibuka mshindi katika soka, Tanzania iliibuka mshindi kwenye Netiboli, Uganda kwenye mpira wa vikapu na Kenya ikashinda tena kwenye mpira wa mikono. Katika riadha, Tanzania ilishinda upande wa wanaume na Kenya ilishinda upande wa wanawake.

Michuano hiyo ambayo imefanyika kwa miaka minane mfululizo katika nchi wanachama, mwaka kesho, imepangwa kufanyika nchini Uganda.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni