.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 30 Agosti 2014

LIGI KUU UINGEREZA KUENDELEA LEO, MANCHESTER UNITED MIKONONI MWA BURNLEY


Ligi kuu nchini Uingereza inaendelea leo katika viwanja mbalimbali, lakini mchezo ambao wengi wanausubiria kwa hamu kubwa ni mchezo kati ya Burnley ambao watakuwa nyumbani kuwaalika Manchester United.

Mchezo huo unangojewa kwa hamu kutokana na rekodi mbovu ya mashetani wekundu tangu kuanza kwa ligi hiyo, kwani katika mchezo wa ufunguzi walikubali kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Swansea, wakatoka sare ya bao 1-1 na Sunderland kabla kuja kukubali kipigo cha mabao 4-0 toka kwa MK Dons katika mchezo wa Capital One.

Ratiba kamili ya mechi za leo na kesho:-

Burnley vs Manchester United (12.45pm)

Manchester City vs Stoke (3pm)

Newcastle vs Crystal Palace (3pm)

QPR vs Sunderland (3pm)

Swansea vs West Brom (3pm)

West Ham vs Southampton (3pm)

Everton vs Chelsea (5.30pm)

Kesho jumapili michezo itakayochezwa ni kati ya:-

Aston Villa vs Hull (1.30pm)

Tottenham vs Liverpool (1.30pm)

Leicester City vs Arsenal

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni