.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 21 Septemba 2014

CRISTIANO RONALDO AONGOZA MAUAJI WAKATI REAL MADRID IKIICHAKAZA DEPORTIVO LA CORUNA

Cristiano Ronaldo amepachika mabao matatu kimiani yaani hat-trick huku akisaidiwa na Gareth Bale kuifanya Real Madrid kuichakaza Deportivo La Coruna kwa mbao 8-2 katika mchezo wa La Liga.

Mshambuliaji huyo raia wa Ureno Ronaldo alipachika kimiani mabao mawili katika kipindi cha kwanza na James Rodriguez kufunga moja na kufanya matokeo kuwa Real kuwa mbele kwa mabao 3-0 hadi mapumziko.

Ronaldo alikamilisha hat-trick yake katika kipindi cha pili, huku mchezaji wa Manchester United aliyotolewa kwa mkopo Real Javier Hernandez akicheka na nyavu mara mbili katika dakika za mwisho. 
  Gareth Bale akifunga goli lake la kwanza kati ya mawili aliyoyapachika wavuni
Chicharito akipongezwa baada ya kufunga goli..nae alicheka na wavu mara mbili

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni