Shehena tani 1.5 ya mikate mibovu
kutoka Kigoma Bakery ikishushwa kwenye dampo la Businde Mkoani
Kigoma tayari kwa kuteketezwa kutokana na kutofaa kwa matumizi ya
binadam shehena hiyo imebambwa kufuatia msako wa kushitukiza wa
(Mamlaka ya chakula na dawaTFDA).
Bidhaa mbalimbali za madukani zikiwa
tayari kwaaajili ya kuteketezwa baada ya muda wake wa matumizi
kuisha,kufuatia msako wa kushitukiza wa TFDA.
Na Editha Karlo, Kigoma
ZAIDI ya Tani 24 za vyakula,dawa za
binaadam na vipodozi zimeteketezwa na mamlaka ya chakula na
dawa(TFDA)katika mikoa minne ya kanda ya katikwasababu ya kutofaa kwa
matumizi ya binaadam.
Akizungumza wakati wa zoezi la
uteketezaji wa bidhaa hizo zilizokamatwa katika zoezi la kustukiza
ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji Mkoani hapa Mkaguzi wa TFDA kanda
ya kati Engliber Bilashoboka alisema kuwa bidhaa hizo zilikamatwa
kati ya Julai mwaka jana na Juni mwaka huu.
Bilashoka alisema kuwa kuteketezwa
kwa bidhaa hizo kunatokana na ukaguzi unaofanywa na maofisa wa TFDA
katika mikoa mbalimbali nchini na lengo likiwa ni kuondoa sokoni
bidhaa zilizoisha muda wake na zisizofaa kwa matumizi ya bindaadam
Alisema pia kufuatia zoezi hilo
mamlaka yake imekifungia kiwanda cha mikate cha Kigoma bekari baada
ya kukutwa na tani 1.5 za mikate mibovu, pamoja na machinjio ya ujiji
kwa kufanya shughuli zake katika hali inayotishia afya za wananchi
Alisema bidhaa hizo zimekamatwa
katika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na dodoma alisema kuwa katika
bidhaa zilikamatwa na kuteketezwa nyingi zilikuwa zikiuzwa huku muda
wake wa kuwa sokoni ukiwa umeisha na zingine zimepigwa marufuku
kuuzwa nchini.
Ofisa huyo alisema kuwa uteketezaji
katika manispaa ya kigoma kwa muda wa wiki moja mpaka sasa ,alisema
mamlaka ya ke imeteketeza zaidi ya tani 4.1zenye thamani ya shilingi
milioni 24 ambavyo havifai kwa matumizi ya binaadamu
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kigoma Ujiji Moses Welansari akizungumzia zoezi hilo alisema kuwa
wamekuwa wakikutana changamoto za wenye maduka zilizokatazwa au
zilizoisha muda wake wa matumizi.
''Elimu imekuwa ikitolewa kwa
wafanyabiasha mara kwa mara ili kuepuka kuweka sokoni bidhaa
zisizotakiwa na mamlaka za serikali na zilizoisha muda wake ''alisema
Kaimu Mkurugenzi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni