FILAMU mpya ya muimbaji wa nyimbo za
Injili, Jennifer Mgendi iitwayo 'Mama Mkwe' inatarajiwa kuigizwa
sokoni siku ya Alhamisi baada ya kukwama kuachiwa jana Jumatatu kama
ilivyokuwa imepangwa.
Aidha Muinjilisti huyo amewataka
mashabiki wake wasiikose kupata darasa la kutosha.
Jennifer alisema filamu hiyo
itaachiwa rasmi Septemba 25 baada ya jana kukwama kwa sababu zilizo
nje ya uwezo wake ikiwa ni wiki kadhaa tangu kumalizika kurekodiwa
kwake na kusema kwa ujumbe uliopo ndani yake, mashabiki hawapaswi
kuikosa.
Muimbaji huyo alisema, kisa cha Mama
anayeingilia ndoa ya mwanae wa kiume akitaka kupatiwa mjukuu ni mambo
ambayo yamekuwa yakiwakumba wanajamii wengi na kusambaratisha ndoa
zao bila kutaka.
"Ni mambo yanayotokea ndaniya
jamii na kuwaachia watu machungu, sasa waigizaji wameonyesha uhalisia
wa mambo namna ndoa nyingi zinavyosambaratika kwa sababu ya mambo
kama hayo," alisema.
Katika filamu hiyo, Jennifer
ameigiza na wasanii wengine wakali kama kina Mussa Banzi, Bahati
Bukuku, Christine Matai, Bibi Esther na wengine.
"Itakuwa mtaani Alhamisi,
mashabiki wasikose kuona uhondo huu. Mama Mkwe ni zaidi ya kazi zangu
za nyuma kwa namna ilivyosukwa na kutendewa haki na wasanii
walioigiza," alitamba Jennifer.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni