.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 12 Septemba 2014

HUKUMU YA KESI YA MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS KUKAMILIKA LEO

Jaji katika kesi inayomkabili mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius leo anatarajiwa kukamilisha kutoa hukumu yake iwapo mwanariadha huyo wa Afrika Kusini alimuua bila ya kukusudia mpenzi wake.

Jaji Thokozile Masipa jana alimsafisha mwanariadha huyo dhidi kosa la kuua kwa kukusudia, kwa kusema wendesha mashtaka walishindwa kudhibitisha alimua kwa makusudi mwanamitindo Reeva Steenkamp mwaja jana.

Pistorius alikiri kufyatua risasi kwenye mlango wa choo chake lakini alisema alidhania kuwa kunamtu kamvamia nyumbani kupitia chooni na wala hakuwa anajua kuwa ni mpenzi wake Steenkamp.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni