Muingereza wa kwanza kupata
maambukizi ya Ebola katika mlipuko wa sasa barani Afrika anatarajia
kurejea katika nchi ambayo ndipo alipopata maambukizo ili kusaidiana
na wenzake kupambana na ugonjwa huo.
Muingereza huyo William Pooley
mwenye umri wa miaka 29 alitibiwa Jijini London baada ya kusafirishwa
kwa ndege kutokea Sierra Leone baada ya kupata maambukizi ya ugonjwa
huo hatari.
Baada ya kupatiwa tiba nyumbani
Uingereza sasa Pooley amepona na kuruhusiwa kutoka hospitali na
amesema anatarajia kurejea Sierra Leone katika wiki chache ili
kusaidia tena kukabiliana na mlipuko wa Ebola.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni