.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 2 Septemba 2014

KAMPUNI YA UBELGIJI YA TPF SAMBRE YAANZA KUFANYA KAZI TANZANIA


Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya ushauri ya TPF Basse Sambre baada kukutana nao leo ofisini kwake Brussels. Wa kwanza kulia ni Bwana. Stefan Pousset Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo na wa kwanza kushoto ni Bwana Jerome Bestgen Meneja wa mauzo wa kampuni hiyo. Wa pili kulia ni Bwana Nyamtara Mukome afisa katika Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji. 

Wawakilshi hao walimweleza Balozi Kamala kwamba wamepata shughuli za kufanya Tanzania na wanatarajia kufungua ofisi zao Tanzania. Balozi Kamala aliwashauri watafute Watanzania wa kushirikiana nao ili kampuni yao iweze kuimarika, kuhimili ushindani katika sekta ya ushauri, kutoa ajira na kusaidia kujenga uchumi wa Tanzania.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni