.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 1 Septemba 2014

LA LIGA MOTO, REAL MADRID YACHAPWA 4-2 NA REAL SOCIEDAD

 Real Madrid imeonja machingu ya ligi kuu nchini Hispania " La Liga " baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-2 toka kwa Real Sociedad katika mchezo uliochezwa jana. 

Pamoja na kutangulia kufunga mabao mawili ya haraka, kibao kiliwageukia mabingwa hao wa klabu bingwa Ulaya na kujikuta wanatandikwa mabao hayo manne. 

Mabao ya Real Madrid yalifungwa Sergio Ramos katika dakika ya 6 na bao la pili likifungwa na Gareth Bale katika dakika ya 11.

Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani mbele ya maelfu ya mashabiki wao, Real Sociedad walizinduka na kuanza kulishambulia lango la Real Madrid na kufanikiwa kupata mabao yao manne kupitia kwa wachezaji Inigo Martinez aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 36, kisha mchezaji David Zurutuza akaifungia timu yake mabao mawili katika dakika za 41 na 65 na bao la nne likiwekwa kimiani na Vela katika dakika ya 76.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni