.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 22 Septemba 2014

LIGI KUU UINGEREZA MANCHESTER CITY 1 CHELSEA 1, FRANK LAMPARD AMSHANGAZA MOURINHO

 Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard alizima kabisa ndoto za kocha Mreno Jose Mourinho na kikosi chake cha Chelsea kuondoka na ushindi wa pointi tatu katika uwanja wa Etihad, pale alipofunga bao la kusawazisha na kufanya matokeo kuwa 1-1 hadi mpira unamalizika. 

Mchezaji huyo mtokea benchi alifunga bao lake la kwanza msimu huu akiwa na Manchester City katika dakika ya 85 ya mchezo huo wa ligi kuu Uingereza uliochezwa jana. 

Chelsea ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 71 ya mchezo, bao hilo likifungwa na Andre Schurrle.
 Mlinda mlango wa Chelsea akiruka bila mafanikio kuokoa mpira uliopigwa na Frank Lampard na kujaa moja kwa moja nyavuni.
SAWA NIMEFUNGA, SISHANGILIII!! Frank Lampard pamoja na kufunga bao hilo muhimu hakuashangilia kama ishara ya heshima kwa Chelsea, timu aliyopata kuichezea kwa mafanikio makubwa na kutwaa mataji mbalimbali.
Zabaleta akizawadiwa kadi nyekundu kutokana na mchezo mbaya

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni