Siku tatu za kutotoka nje ili
kudhibiti mlipuko wa Ebola nchini Sierra Leone zimeelezwa kuwa
zimekuwa na mafanikio na mamlaka za nchi hiyo.
Agizo hilo la kutotoka nje katika
maeneo mengi ya nchi hiyo limemalizika jana usiku, na halitaongezwa
muda kwa mujibu wa mamlaka za Sierra Leone.
Sierra Leone ni moja ya nchi ambazo
zimeathiriwa mno na mlipuko wa Ebola, ikiwa na vifo 550 kati ya vifo
2,600 vilivyotokea hadi sasa.
Wakati huo huo nchi ya jirani ya
Liberia imetangaza kuongezeka mara nne kwa wagonjwa waliolazwa
kutokana na mlipuko wa Ebola.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni