Uturuki imeanza kufunga mipaka yake
na Syria baada ya wakimbizi 70,000 wa Kikurdi kuingia nchi hiyo siku
ya Ijumaa.
Hali hiyo imechangiwa na mapambano
ya siku ya Jumapili baina ya vikosi vya usalama vya Uturuki na
Wakurdi waliokuwa wanapingana nao.
Kufungwa kwa mipaka kutawazuia
Wakurdi walio Uturuki kurejea Syria kupambana na wapiganaji wa kundi
la Dola ya Kiislam (IS).
Wengi wa wakimbizi wanaotokea mji wa
Kobane, wamekimbia mauaji yanayofanywa na wapiganaji wa kundi la IS
ambao wamekuwa wakisonga mbele kuutwaa mji huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni