.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 19 Septemba 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA MPANGO WA UTAMBUZI WA UJUZI ULIOPATIKANA NJE YA MFUMO RASMI WA MAFUNZO JIJINI DAR LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kama ishala ya kuzindua rasmi mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Kazi, na Ajira, Gaudensia Kabaka (kushoto) ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dkt. Shukuru Kawambwa.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, mmoja kati ya wahitimu 30, wa mafunzo hayo, Charles Gwambassa, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali. Hafla hiyo ilifanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti, mmoja kati ya wahitimu 30, wa mafunzo hayo, Mwajuma Massoud, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango wa Utambuzi wa ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa mafunzo, kwa ajili ya kutathimini na kutambua ujuzi na elimu ua ufundi Stadi kwa Vijana waliojifunza fani mbalimbali Hafla hiyo ilifanyika leo Septemba 19, 2014 kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni