.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 12 Septemba 2014

MFUNGWA ALIYEWAUWA WANAFUNZI WATATU ATOROKA GEREZANI NCHINI MAREKANI

Msako umeanza huko Lima, Ohio nchini Marekani baada ya kijana mmoja nchini Marekani ambaye aliwapiga risasi na kuwauwa wanafunzi watatu, kutoroka gerezani.

Kijana huyo TJ Lane, 19, anatumikia adhabu ya vifungo vitatu vya maisha baada ya kukiri kosa la mauaji katika shule ya Chardon Februari 2012.

Polisi wamesema mfungwa mwingine aliyetiwa hatiani kwa kosa wizi, Clifford Opperud, pia naye ametoroka katika tukio hilo.

Mamlaka za Marekani zimesema haziamini kama wafungwa hao wanasilaha lakini wawili hao ni watu hatari.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni