.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 12 Septemba 2014

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MH. MATHIAS CHIKAWE AWASILI MKOANI KIGOMA NA KUKUTANA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya (kushoto) akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe katika ofisi za Mkoa huo zilizopo mjini Kigoma wakati Waziri Chikawe na maafisa wake walipofanya ziara ya kikazi katika mkoa huo. Waziri Chikawe alikutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya usalama katika wilaya zote za mkoa huo. Waziri Chikawe katika ziara yake hiyo, pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama katika Ukumbi wa Ofisi yake. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ambaye pia alishiriki katika kikao hicho kilichokuwa kinajadili masuala mbalimbali ya usalama mkoani Kigoma. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani hum leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa huo pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kikao kilichoitishwa kwa ajili yake, na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Luteni Kanali Mstaafu, Issa Machibya. Katika kikao hicho kilichofayika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi za Mkoa wa Kigoma, Waziri na Kamati hiyo walijadiliana masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama. Waziri Chikawe na maafisa wake waliwasili mkoani humo leo kwa ajili ya ziara ya kikazi. Waziri Chikawe licha ya kukutana na Kamati hiyo ya mkoa, pia anatarajiwa kutembelea Kambi za Wakimbizi zilizopo mkoani humo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni