Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere (kushoto) akifuatilia maonyesho
mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa Tamasha la 33
la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo
(TaSUBa) jana, katikati ni Mtendaji mkuu TaSUBa Bw. Michael J.
Kadinde na kulia ni Mkurugenzi Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas
Mwansoko.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kati akipiga ngoma kama ishara ya
uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana.
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Makongoro Nyerere kulia akipokea zawadi ya picha
kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TaSUBa Bw. Ghonche Materego wakati
wa uzinduzi wa Tamasha la 33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya
Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) jana. Picha hii imechorwa sura
ya Mhe. Makongoro na msanii aliyefaamika kwa jina la Sunday Richard
Kamangu.
Wasanii kutoka Taasisi ya Sanaa na
Utamaduni Bagamoyo wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa Tamasha la
33 la Sanaa lililofanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo (TaSUBa) jana. (Picha zote na: Genofeva Matemu – MAELEZO).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni