.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 22 Oktoba 2014

BAYERN MUNICH YAIGARAGAZA ROMA MABAO 7-1 LIGI YA MABINGWA ULAYA

Ligi ya mabingwa Barani Ulaya imeendelea usiku wa kuamkia leo kwa kushuhudia vinara wa ligi kuu nchini Ujerumani, Bayern Munich wakiishushia kipigo kikali Roma cha mabao 7-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Stadio Olimpico nchini Italia.
Ikiwa na kikosi chake cha mauaji, Bayern walipata mabao yao kupitia kwa Arjen Robben aliyefunga mabao mawili katika dakika za 9 na 30, bao la tatu likafungwa na Mario Gotze katika dakika ya 23, bao la nne likawekwa kimiani na Lewandowski katika dakika ya 25 ya mchezo huku bao la tano likifungwa na Thomas Muller kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 35. 

Bao la sita lilifungwa na Frank Ribery katika dakika ya 78 na bao la saba likawekwa kimiani na mchezaji Shaqiri katika dakika ya 80 ya mchezo huo. 

Bao la kufutia machozi la Roma lilifungwa na Gervinho katika dakika ya 66.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni