.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 22 Oktoba 2014

LIGI YA MABINGWA ULAYA, CHELSEA YAPIGA 6-0 DHIDI YA MARIBOR, NAZO BARCELONA, SCHALKE, SHAKTAR ZAFANYA MAUAJI

 Matajiri wa jiji la London, timu ya soka ya Chelsea usiku wa kuamkia leo waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Maribor katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, mchezo uliochezwa Stamford Bridge.
 Chelsea ambao ndio vinara wa ligi kuu nchini Uingereza mpaka sasa, walijipatia mabao yao kupitia kwa wachezaji Loic Remy aliyefunga bao la kwanza, Didier Drogba alifunga bao la pili kwa mkwaju wa penati na bao la tatu likawekwa kimiani na mkongwe John Terry. 

Bao la nne na Chelsea liliwekwa kimiani na mchezaji Viler wa Maribor ambaye alijifunga akiwa katika harakati za kuondoa hatari langoni mwake. Eden Hazard akaifungia timu yake bao lingine kwa mkwaju wa penati.
 Katika mchezo mwingine wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, FC Barcelona waliutumia vyema uwanja wao wa Nou Camp baada ya kuifunga Ajax toka Uholanzi kwa jumla ya mabao 3-1. 

Mabao ya vinara hao wa ligi kuu nchini Hispania " La Liga " yalifungwa na wakali wake Neymar katika dakika ya 8 ya mchezo huku Lionel Messi akifunga bao la pili katika dakika ya 24 na bao la tatu likiwekwa kambani na Ramirez katika dakika ya 90 ya mchezo. 

Bao la kufutia machozi la Ajax lilifungwa na El Ghazi katika dakika ya 88 ya mchezo.
Matokeo mengine ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, mechi zilizochezwa usiku wa kumakia leo:-

Apoel Nicosia 0 vs 1 PSG

Schalke 4 vs 3 Sporting Lisbon

BATE 0 vs 7 Shaktar Donetsk

FC Porto 2 vs 1 Athletico Bilbao

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni