Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrissa Mshoro
akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mpango wa chuo hicho wa
kuendelea na jitihada za kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na tanga ngumu
ikiwemo ujengaji wa miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia
zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji na
gesi asili ya kupikia, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa chuo hicho Prof.
Gabriel Kassenga.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye pia ndiye mtaalam wa
teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka (waste treatment
facilities) Dkt. Shabaan Mgana Akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani)
namna Teknolojia hiyo ya kubadili taka ngumu na maji taka inavyotumika na
kuwasaidia wananchi walioonesha nia ya kuitumia ikiwamo kupata mboji kwa ajili
ya mazao, mimea pamoja na kupata gesi asili ya kupikia, ambapo mpaka sasa kiasi
cha nyumba 100 za awali katika mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na nyumba mia
moja katika Chuo Kikuu cha Ardhi zimeshaunganishwa katika Mradi huo, wakati wa
mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mkuu
wa Chuo hicho Prof. Idrissa Mshoro.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo na
kutembelea maeneo ilipojengwa miundombinu ya teknolojia za kibiolojia
zinazobadili taka ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza Selele akiwasha
karatasi kwa kutumia Gesi Asili iliyozalishwa na Mtambo huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni