Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini
Oscar Pistorius anapaswa kupatiwa adhabu ya kutosha kwa kumuua mpenzi
wake Reeva Steenkamp, binamu wa marehemu ameiambia mahakama.
Binamu huyo Kim Martin ameiambia
mahakama ya Pretoria kuwa Pistorius anapaswa kuadhibiwa kwa kosa
alilolifanya.
Upande wa mashtaka umekuwa ukijenga
hoja za kuhakikisha Pistorius anafungwa kifungo jela.
Pistorius alitiwa hatiani mwezi
uliopita kwa kosa la kuua bila ya kukusudia na anakabiliwa na
uwezekano wa kifungo cha miaka 15 jela, ingawa jaji anaweza pia
kutomfunga na kumuamuru kulipa faini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni