KIKAO cha Secretarieti ya Coastal Union kilichoketi jana usiku kimetua
majina ya watu watano watakaosimamia Uchaguzi Mdogo wa Klabu hiyo unatarajiwa kufanyika Novemba 23 mwaka huu ili kuweza kuziba nafasi za uongozi zilizokuwa wazi.
Baada ya majina hayo kuteuliwa yatawasilishwa kwenye shirikisho la
soka nchini (TFF) kwa ajili ya taratibu nyengine ambapo itaanza
kutangaza tarehe ya uchukuaji fomu na urudishaji fomu mara baada ya
taratibu mbalimbali kumalizika.
Uchaguzi huo unafanyika ili kuweza kujaza nafasi tatu zilizokuwa wazi
ambazo ni Mwenyekiti na Wajumbe wawili wa kamati ya utendaji lengo
likiwa kuharakisha maendeleo ya Coastal Union.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kikao hicho,Katibu Mkuu wa
Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa kamati hiyo iliyoteuliwa
wana uwezo mzuri wa kusimamia chaguzi mbalimbali mkoani hapa.
“Kimsingi walioteuliwa wana uwezo mzuri lakini lazima majina hayo
tuyapelekea TFF kwa ajili ya taratibu nyengine zinazofuata na baadae
watae watangaze tarehe ya uchukuaji fomu na urudishwaji fomu tayari
kwa ajili ya uchaguzi huo “Alisema El Siagi.
Aliyataja majina yaliyopendekezwa kwenye kikao hicho ambao watakuwa
chini ya Mwenyekiti wake Abdallah Yahaya,Katibu Mohamed Awadhi na
wajumbe wake watakuwa ni Mtwana Akida Boramini,Ibrahim Khatibu na John
Joba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni