Bondia Tomas Mashali
kushoto akijifua wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia
Henry Wandera kutoka kenya novemba 1 katika ukumbi wa friends corner manzese,
akisimamiwa na Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve (Picha na
www.superdboxingcoach.blogspot.com)
BONDIA Thomasi Mashali
yupo katika maandalizi mazito ya kumkabili bondia kutoka kenya Henry
Wandera Novemba mosi katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam
Akizungumza wakati wa mazoezi yake juzi Mashali amesema kuwa
yupo fiti wakati wowote yeye kufanya kazi hivyo haofii hata kidogo mpambano huo na
kuwataka mashabiki wake waje waone anavyo mgalagaza vibaya sana siku hiyo
mkenya Wandera
Mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano
mengine ya utangulizi yatakayo wakutanisha Mbayo Ilunga na Fred Sayuni wakati
Joseph Mbowe ataoneshana umwamba na Saidy Salum na Ramadhani Johncena
ataoneshana ubabe na Baina Mazola
Mapambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita
katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha
kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo kingilio ni shilingi, 7000; kwa kila mtu
mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo
zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika mchezo huo
Pia kunakuwa na
mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na
mabambano ya ngumi ya ndani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni