.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Oktoba 2014

KIJANA APIGWA MAWE HADI KUFA NCHINI SOMALIA KWA KOSA LA KUMBAKA MWANAMKE

Mahakama ya Kislam imetekeleza hukumu ya kupigwa mawe hadi kufa kwa kijana mmoja kusini mwa Somalia, baada ya kumtia hatiani kwa kubaka mwanamke, taarifa za tovuti ya Kiislam imeeleza.

Jaji aliagiza kijana Hasan Ahmad Ali mwenye umri wa miaka 18, kumlipa fidia mwanamke huyo huyo ndama mmoja, na kisha baadae kijana huyo kuuwawa.

Katika kesi hiyo kijana Ali alikanusha kumbaka mwanamke huyo Fadumo Hasan Mohmoud mwenye umri wa miaka 28.

Mwezi uliopita mwanamke mmoja alipigwa mawe hadi kufa katika bandari ya Barawe, baada ya mahakama ya Kiislam kumtia hatiani kwa kuolewa na wanaume wanne kwa wakati mmoja.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni