.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 23 Oktoba 2014

DAKTARI ASEMA MICHAEL SCHUMACHER ATAPONA NDANI YA MIAKA MITATU

                                                          Schumacher akiwa na mkewe Corinna

Daktari wa Ufaransa aliyemtibu bingwa wa mbio za magari za Langalanga Michael Schumacher baada ya kupata ajali wakati akiteleza kwenye barafu, amesema anaweza akapona ndani ya miaka mitatu.

Daktari Jean-Francois Payen, wa hospitali ya Grenoble alimtibu Schumacher baada ya kuumia Desemba 2013, ameitembelea familia ya Schumacher katika nyumba yao iliyopo nchini Switzerland.

Schumacher (45) anatibiwa akiwa nyumbani baada ya kukaa miezi sita akipatiwa tiba bila ya fahamu kufuatia ajali hiyo aliyoipata huko Meribel nchini Ufaransa.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni