Shirikisho la kandanda nchini Nigeria limemtangaza Shaibu Amodu kuwa kocha mkuu wa kikosi cha timu ya soka la taifa hilo " Super Eagles " kuchukua nafasi ya Stephen Keshi.
Maamuzi hayo yamekuja saa kadhaa baada ya Keshi ambaye amekuwa akiifundisha timu hiyo ya taifa bila kuwa na mkataba, kuiongoza Nigeria hapo jana kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sudan katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
Mkataba rasmi kati ya kocha huyo na Shirikisho la Soka la Nigeria unatarajiwa kufanywa baada ya michezo miwili iliyosalia dhidi ya Congo ambao Nigeria watakuwa ugenini na ule wa nyumbani dhidi ya Afrika Kusini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni