Idadi ya watalii
wa kimataifa wanaowasili nchini Kenya, imeshuka kwa asilimia 13.1
katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, kufuatia mashambulio yanayofanywa
wapiganaji wa al-Shabaab wa Somalia.
Takwimu rasmi za
Bodi ya Utalii Kenya, zimesema watalii walioingia Kenya katika miezi
sita hadi Juni ni 428,585 ikilinganishwa na watalii 495,978 katika
kipindi kama hicho mwaka jana.
Aidha
ikilinganishwa na mwaka 2012, idadi ya watalii waliongia nchini Kenya
katika kipindi cha Januari hadi Juni imeshuka kwa asilimia 24.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni