Waziri wa Elimu Jacob Kaimenyi
(kulia) akiwa na Katibu Mkuu Belio Kipsanga pamoja na Mwenyekiti wa
Baraza la Taifa la Mitihani Kenya Kabiru Kin yanjui.
Mitihani ya taifa Kenya inayoaminika
kuwa ndio ambayo wanafunzi wataifanya wiki ijayo siku ya jumanne
inauzwa wazi wazi katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo.
Baraza la Taifa la Mitihani Kenya
jana limetangaza vituo vya mitihani vya Garissa, Kisii, Oyugis,
Nyamira, Rongo na Eastleigh huko Nairobi kuwa ndio huwa vinaongoza
kwa wizi wa mitihani.
Kauli hiyo ya baraza la taifa la
mitihani Kenya imekuja baada ya mwanafunzi wa Chuo Kukuu cha Kenyatta
kukamatwa katika kaunti ya Nyamira, akiwa na mitihani kwenye flashi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni