Shirika la Afya Duniani (WHO)
itaongeza jitihada za kudhibiti ugonjwa wa Ebola usisambae nje ya
nchi tatu za Afrika zilizoathiriwa zaidi na ugonjwa huo hatari.
Nchi 15 za Afrika zimepewa
kipaumbele, afisa wa ngazi ya juu wa WHO, Isabbele Nutall ameuelezea
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Geneva.
Nutall amesema mataifa hayo
yatapatiwa msaada zaidi wa kudhibiti na kinga katika jitihada za
kukabiliana na Ebola.
Hata hivyo Katibu Mkuu wa zamani wa
Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan amesema amekasirishwa mno na namna
Jumuiya ya Kimataifa ilivyozorota kusaidia kudhibiti Ebola.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni