.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 2 Oktoba 2014

NSSF YACHANGIA VIFAA VYA ICU HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI


Kutoka kushoto ni Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Devota Ikandilo, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji, Dk John Kimario, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Marina Njelekela na Ofisa Uhusiano wa NSSF, Jumanne Mbepo katika picha ya pamoja baada ya NSSF kukabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 20 kwa ajili ya kununulia vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Jumanne Mbepo (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi ya sh. milioni 20 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Marina Njelekela kwa ajili ya kununulia vifaa vya chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umechangia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Msaada huo utatumika kununulia vifaa kwa ajili ya chumba cha Wagonjwa mahututi (ICU).

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili  Dk. Marina Njelekela aliishukuru NSSF kwa msaada huo na kuongeza kuwa msaada huo utaenda kuokoa maisha ya watanzania wengi.

Pia aliwashauri NSSF kushiriki kwenye clinic Maalumu ya upimaji wa Kansa ya Matiti kwa kina mama ambalo hufanyika hospitalini hapo.

Nae  Mwakilishi wa NSSF, Jumanne Mbepo alisema kua mchango uliotolewa na NSSF kwa hospitali hiyo hautoshi kununua vifaa vyote na kuomba Taasisi
nyingine ziichangie Hospitali hiyo ili kuweza kuokoa maisha ya
Watanzania wengi zaidi.

NSSF imekuwa ikitoa huduma ya bima ya  Afya kwa wanachama wake ijulikanayo kama SHIB , Hospitali ya muhimbili  ni mojawapo ya watoa huduma wa bima hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni