.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 19 Oktoba 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE NA RAIS JOSEPH KABILA WAONGOZA SHEREHE ZA KUHITIMU MAAFISA WAPYA WA JESHI

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maofisa wa Jeshi wanafunzi kundi la 54/13 DRC katika chuo cha Mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha jana Jumamosi Oktoba 18, 2014.

Maafisa wapya wa jeshi la Wananchi wa Tanzania wakila kiapo cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi la wananchi wa Tanzania iliyofanyika katika chuo cha mafunzo ya kijeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha.

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) akimpa zawadi ofisa kadeti Yusup kutoka DRC baada ya kuibuka mwanafunzi bora katika kundi la 54/13 wakati wa hafla ya kumaliza mafunzo iliyofanyika huko Monduli jana.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakijadili jambo wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Joseph Kabila wa DRC na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wakisimama kikakamavu wakati nyimbo za taifa za nchi hizo zikipigwa wakati wa hafla ya kuhitimu mafunzo na kutunuku kamisheni kwa maafisa wa kundi la 54/13 DRC yaliyofanyika chuo cha kijeshi Monduli Mkoani Arusha. Picha na Fred Maro.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni