.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 18 Oktoba 2014

SSRA YAJIPANGA KUBORESHA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Irene Isaka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu hatua zilizochukuliwa na mamlaka hiyo katika kuboresha sekta ya Hifadhi ya Jamii hapa nchini. Kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA Bi. Sarah Kibonde Msika.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bw. Ngabo Ibrahimu(Katikati)akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu maboresho ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii na Miongozo iliyotolewa na Mamlaka hiyo inayolenga kuboresha sekta ya Hifadhi ya Jamii.Kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji Bi. Sarah Kibonde Msika na Kulia ni Mkurugenzi wa Usajili na Matekelezo wa SSRA Bi. Lightness Mauki.
Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi. Sarah Kibonde Msika akieleza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mikakati ya Mamlaka hiyo katika kutetea na kulinda maslahi ya wanachama ikiwemo kuboresha Kikokotoo cha Mafao ya Pensheni.Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kutoka SSRA Bw. Ngabo Ibrahimu.

Baadhi ya waaandishi wa habari wakiwasikiliza wawasilishaji kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) wakati wa Mkutano uliofanyika leo kwenye Ofisi za Mamlaka hiyo Jijini Dar Es Salaam.

                                                                                            Picha na Fatma Salum

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni